Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uhalifu: Pikipiki zisizo na namba zikamatwe – Madereva Bodaboda

IMG 20240227 WA0023 Uhalifu: Pikipiki zisizo na namba zikamatwe – Madereva Bodaboda

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: Dar24

Kutokana na matukio mengi ya mauwaji ya Madereva wa Pikipiki maarufu kama Bodaboda ndani ya kipindi kifupi, Mkuu wa kituo cha Polisi Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, ASP Amiri Mlemba ametembelea vijiwe vya bodaboda na kutoa elimu ya namna ya kukabiliana na abiria wahalifu.

Mlemba ameamua kutembelea vijiwe hivyo ili kuwaelimisha na kuwaeleza kwamba Polisi itaendelea kufanya Wilaya nzima, ili kuhakikisha mauji hayo yanadhibitiwa na kumalizika kabisa.

Kwa upande wao baadhi ya Madereva Bodaboda wameliomba Jeshi la Polisi kufanya msako wa Pikipiki zote ambazo hazina namba za usajili ili zikamatwe, kwani wanahisi zinakuwa chanzo cha uhalifu wa matukio

Chanzo: Dar24