Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ugomvi wa Kuku watatu wasababisha mauaji

0c63cdf42ed8c02188130d1768ca7321.jpeg Ugomvi wa Kuku watatu wasababisha mauaji

Thu, 4 Nov 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WANANCHI wamewaua watu wawili katika kijiji cha Ikunguigazi wilayani Mbogwe, mkoani Geita kwa kuwapiga na kisha kuwachoma moto kwa tuhuma za kuiba kuku watatu.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Dismas Kisusi alisema jana kuwa tukio lilitokea Oktoba 29, saa moja asubuhi wakati watuhumiwa walipokutwa na jogoo wawili na tetea mmoja.

Kamanda Kisusi aliwaeleza waandishi wa habari kuwa mmoja wa marehemu ametambulika kwa jina la Mambo Elias (18) na alikuwa mkulima na mkazi wa kijiji cha jirani cha Lulembela na mwingine hajafahamika.

"Wenzao wawili ambao walikuwa pamoja walikimbia baada ya kuona wenzao wamekamatwa na wananchi wenye hasira,” alisema na kuongeza;

"Jeshi la polisi mkoani Geita linawashikilia watu watatu kuhusiana na tukio hili akiwemo mwenyekiti wa kijiji cha Ikunguigazi, Jumanne Richard (41). Wengine ni viongozi wa sungusungu kijijini hapo, Bunzali Mbapula (50) na Joseph Malunguja (30)."

Chanzo: www.habarileo.co.tz