Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ugomvi na Mbunge.... Diwani auawa kwenye mkutano

Diwani Nyieee.jpeg Stephen Maloba enzi za uhai wake

Sun, 2 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Diwani (MCA) wa Kisa Mashariki nchini Kenya, Stephen Maloba amefariki dunia baada ya wahuni kumvamia na kumdunga na kisu kwenye farakano baina ya upande wake na wa mbunge wa Khwisero Christopher Aseka.

Polisi Kakamega wamethibitisha kifo cha MCA huyo wa kujitegemea.

“Nina habari za kifo cha diwani kilichotokea Khwisero lakini bado ninakusanya mengi kuhusu kilichotokea,” Kamanda wa Polisi Kaunti ya Kakamega Joseph Kigen amesema.

Gavana wa Kakamega Fernandes Barasa amelaani mauaji hayo lakini pia akawataka wakazi na wenyeji wa kaunti hiyo waishi kwa amani.

Seneta wa Kakamega Dkt Boni Khalwale ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter akithibitisha kifo cha Bw Maloba.

“Niko katika mochwari ya Hospitali ya Mbale nikishughulika baada ya diwani wa Kisa, Mheshimiwa Maloba kuuawa kwa kudungwa kwenye mzozo na Mheshimiwa Aseka ambaye ni Mbunge wa Khwisero,” ameandika Seneta Khalwale.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live