Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura amedai kuwa uchunguzi uliyofanywa na Jeshi la Polisi umebaini kwamba Hamza Mohammed alikuwa gaidi wa kujitoa mhanga.
"Katika uchunguzi wetu tumeweza kubaini,Hamza Mohamed, amekuwa akijifunza mambo mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii, kwa kipindi kirefu amekuwa akijifunza mambo ya ugaidi, kwa kuangalia mitandao inayoonesha matendo ya Al-Shabab lakini pia matendo ya vikundi kama ISS, uchunguzi wetu umebaini Hamza ni Gaidi"-DCI Wambura
Hamza aliuawa na polisi Agosti 25, mwaka huu baada ya kuwaua kwa risasi askari wanne, watatu kati yao wa polisi na mmoja wa kampuni binafsi ya ulinzi jirani na ulipo ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam.