Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uamuzi mdogo kesi ya Ole Sabaya leo

Cctv Sabaya Uamuzi mdogo kesi ya Ole Sabaya leo

Mon, 3 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha leo Jumatatu Januari 3, 2022 imepanga kutoa uamuzi mdogo wa pingamizi lililowasilishwa na mawakili wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita.

Pingamizi hilo liliwasilishwa wakati shahidi wa 13 wa Jamhuri ambaye ni Ofisa Uchunguzi kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru), Ramadhan Juma akitoa ushahidi.

Hata hivyo, Desemba 29 mwaka jana, mahakama hiyo ilishindwa kutoa uamuzi huo baada ya mawakili wa utetezi kushindwa kufika mahakamani.

Itakumbukwa, Desemba 17 mwaka jana, akiwasilisha hoja ya pingamizi hilo Wakili Mosses Mahuna aliieleza kuwa shahidi huyo hana uwezo wa kutambua watu kupitia ripoti ambayo hajaiandaa na wala si mtaalamu kutoka maabara ya kiuchunguzi.

Hata hivyo, mawakili wa Serikali waliomba mahakama kutupilia mbali pingamizi hilo, kwani halina misingi ya kisheria wala mashiko. Hakimu Mkazi, Patricia Kisinda aliahirisha kesi hiyo hadi leo atakapotoa uamuzi huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live