Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uamuzi Mdogo Kesi ya Sabaya Wakwama

Cctv Sabaya Uamuzi Mdogo Kesi ya Sabaya Wakwama

Wed, 29 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha leo Jumatano Desemba 29, 2021 imeshindwa kutoa uamuzi mdogo katika kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita baada ya mawakili wa utetezi kushindwa kufika mahakamani.

Kutokana na mawakili hao wa watetezi kushindwa kufika mahakamani sasa maamuzi hayo yatatolewa Januari 3,2022.

Watuhumiwa hao wanatetewa na Mawakili Mosses Mahuna, Fauzia Mustafa, Edmund Ngemela, Sylvester Kahunduka na Fridolin Bwemelo.

Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 27 ya mwaka huu, mbali na Sabaya watuhumiwa wengine ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Patricia Kisinda upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Felix Kwetukia na Mwendesha Mashitaka wa Takukuru, Jacob Piyo.

Wakili Kwetukia alieleza mahakama kuwa upande wa watuhumiwa hakuna wakili hata mmoja na watuhumiwa wote wapo mbele ya mahakama hiyo hivyo mahakama inakuwa haipo katika nafasi ya kutoa uamuzi huo mdogo labda kama washitakiwa wataondoa uwakilishi.

Kufuatia hali hiyo, Hakimu Kisinda, aliwauliza watuhumiwa hao iwapo bado wanauwakilishwa na mawakili wao ambapo waliieleza mahakama bado wanawakilishwa.

Uamuzi huo mdogo ulipangwa kutolewa baada ya mawakili wa utetezi kuwasilisha pingamizi kutolewa shahidi wa 13 wa Jamhuri, Ofisa Uchunguzi kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru),Ramadhan Juma, akiendelea kutoa ushahidi.

Desemba 17 mwaka huu, akiwasilisha hoja ya pingamizi hilo Wakili Mahuna aliieleza mahakama kuwa shahidi huyo hana uwezo wa kutambua watu kupitia ripoti hiyo ambayo hajaiandaa yeye na wala siyo mtaalamu kutoka maabara ha kiuchunguzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live