Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tume ya walimu yalivalia njuga sakata la mwalimu anayedaiwa kuua mwanafunzi Bukoba

Thu, 30 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) imemuagiza Kaimu Katibu Msaidizi wa tume hiyo Wilaya ya Bukoba kuchukua sheria dhidi ya Mwalimu Respecious Patrick wa shule ya Msingi ya Kibeta Manispaa ya Bukoba, anayedaiwa kumpiga hadi kufa mwanafunzi Sperius Eradius.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 30, Katibu wa Tume hiyo Winifrida Rutaindurwa amesema kuna haja ya kufungua mashauri ya kinidhamu kwa walimu wa shule hiyo ili sheria ichukue mkondo wake.

“Lakini nitumie nafasi hii kuwataka walimu wote kuhakikisha wanazingatia sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza katika kutoa adhabu ya viboko kwa wanafunzi" amesema Rutaindurwa.

Ameongeza: “Nimejiuliza hadi mwalimu anachukua hatua hiyo kuna uwezekano mkubwa amekuwa na tabia ya kuwaadhibu wanafunzi kupita kiasi.”

Sijaelewa kwanini uongozi wa shule haukuchukula hatua za kinidhamu kwa kuwa mwalimu Mkuu ndiye mwenye mamlaka ya kwanza ya nidhamu kwa walimu, kwa mujibu wa Sheria.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz