Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuhuma za wizi; RC aagiza kigogo wa halmashauri akamatwe

42093 Pic+kigogo Tuhuma za wizi; RC aagiza kigogo wa halmashauri akamatwe

Mon, 18 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Songea. Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme ameliagiza jeshi la polisi kumkamata na kumweka ndani saa 48 na kumfikisha mahakamani kigogo mmoja wa idara ya fedha halmashauri ya manispaa ya Songea kwa tuhuma za wizi wa fedha za mapato Sh118 milioni.

Pia ameagiza maofisa wawili wa ngazi za juu wanaoshughulika na masuala ya fedha katika halmashauri hiyo wasimamishwe kazi mara moja kupisha uchunguzi zaidi.

Mkuu huyo wa mkoa amedai kigogo huyo wa idara ya fedha ameiba fedha hizo katika kipindi cha miezi mitano ambapo alikua akichukua kidogo kidogo na kukopesha wenzike na kuisababishia halmashauri hasara kubwa.

“Kama kuna mtumishi yeyote ambaye anajinufaisha na kuiba fedha za mapato ya halmashauri achukuliwe hatua mara moja, hatuwezi kufumbia macho tatizo hili, naagiza asakwe popote alipo na kufikishwa mahakamani RPC (Mkuu wa polisi mkoa) mweke ndani saa 48 kisha mfikishe mahakamani wakati taratibu zingine za kisheria zikiendelea, fedha hizo zingeweza kuwasaidia wananchi kujengewa wodi ya kujifungulia wajawazito au hata madarasa.”

“Mkurugenzi naye achukue hatua za nidhamu kulingana na taratibu za sheria na kuendelea kuwa jasiri kwa kutofumbia macho vitendo vya wizi na ubadhirifu,” alisema.

Mkuu huyo wa mkoa alisema pia amemsimamisha kazi mkuu wa idara hiyo kwa kushindwa kubaini wizi huo mapema wakati ndiye msimamizi mkuu wa mapato yote ya halmashauri hiyo.



Chanzo: mwananchi.co.tz