Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuhuma za kuwapa mimba wanafunzi, 10 mbaroni wamo walimu, diwani CCM

29703 Mimba+pic TanzaniaWeb

Mon, 3 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Geita. Polisi wilaya ya Nyang'hwale mkoani Geita linawashikilia watu 10 wakiwamo walimu wanne na diwani wa CCM kwa tuhuma za wanafunzi kupata ujauzito.

Hatua hiyo ya polisi kuwakamata watuhumiwa hao, inatokana na agizo la Naibu Waziri  wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mwita Waitara la jana Ijumaa aliloagiza wale wote waliowapa mimba wanafunzi wilayani humo wakamatwe.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi mkuu wa wilaya hiyo, Hamimu Gwiyama amesema kazi ya kuwakamata ilianza jana usiku na bado inaendelea.

Amesema hadi asubuhi ya leo Jumamosi wamekamatwa walimu wanne, diwani wa CCM, mtendaji wa kijiji na wengine wanaodaiwa kuwapa mimba wanafunzi.

Mkuu huyo wa wilaya amesema diwani amekamatwa baada ya mtoto wake kupata ujauzito lakini yeye na mwanae hawakwenda kutoa ushahidi mahakamani na kusababisha kesi kushindwa.

Amesema kazi ya kuwasaka wote waliowapa mimba wanafunzi na wanaoharibu ushahidi inaendelea na sheria lazima ichukue mkondo wake.



Chanzo: mwananchi.co.tz