TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imethibitisha kuwa inamshikilia mfanyabishara Yusuf Manji kwa mahojiano kuhusu tuhuma mbalimbali tatu zinazomkabili.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna wa Polisi, Salum Hamdun amesema kuwa Manji ambaye amerejea nchini karibuni baada ya kuondoka tangu mwaka 2018 anatuhumiwa kwa makosa matatu.
CP Hamdun amesema tuhuma hizo zinahusisha kampuni zake za Intertrade Commercial Ltd Serivice na Golden Globe International Service Limited.
Tuhuma ya kwanza ni kuisababishia serikali hasara kwa kukwepa kulipa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na udanganyifu wakati akifanya biashara na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Pili, inadaiwa kuwa kupitia kampuni ya Golden Globe alifanya udanganyifu wakati wa kununua hisa za kampuni ya mawasiliano ya Tigo.
Tatu ni tuhuma ya mapato ya Yanga SC yanayohusu kampuni ya Quality Group. Manji alikamatwa juzi katika uwanja wa ndege mara baada ya kuwasili nchini.