Sarafu za Bitcoin iliyoibiwa yenye thamani ya zaidi ya $5bn (sawa na Tsh Trilioni 115.700) imekamatwa na Idara ya Haki ya Marekani na kueleza kwamba ukamataji huo ni mkubwa zaidi kuwahi wa aina yake kuwahi kutokea duniani.
Maafisa pia waliwakamata na kuwafungulia mashtaka watu wawili siku ya Jumanne kwa kujaribu kutakatisha pesa hizo, ambazo ni sawa na karibu 120,000 Bitcoin.
Fedha hizo, zilizoibiwa na mdukuzi ambaye alikiuka ubadilishanaji wa sarafu fiche mwaka wa 2016, zilikuwa na thamani ya takriban $71m. Lakini, pamoja na kupanda kwa thamani ya Bitcoin, sasa ina thamani ya zaidi ya $5bn.
Msaidizi wa Mwanasheria Mkuu Kenneth Polite Jr alisema kunaswa huko kulikuwa dhibitisho kwamba serikali "haitaruhusu sarafu fiche kuwa mahali salama pa ufujaji wa pesa au eneo la uvunjaji sheria ndani ya mfumo wetu wa kifedha".
Pesa hizo zilitokana na udukuzi wa mwaka wa 2016 wa ubadilishanaji wa crypto unaojulikana kama Bitfinex.
Kulingana na maafisa wa Idara ya Haki, mdukuzi alivunja jukwaa, akafanya zaidi ya miamala 2,000 ambayo haijaidhinishwa na kisha kuingiza pesa hizo kwenye pochi ya kidijitali inayodaiwa kuendeshwa na Ilya Lichtenstein, 34, wa New York.