Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Trafiki wawili wadaiwa kumpora Mchina Sh mil 19 na kusahau kofia yao

Trafiki Polisi Trafiki wawili wadaiwa kumpora Mchina Sh mil 19 na kusahau kofia yao

Sun, 20 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Askari wawili wa usalama barabarani nchini Kenya wanaripotiwa kumwpora raia mmoja wa China shilingi milioni moja za Kenya (sawa na shilingi milioni 19 za Kitanzania), Alhamisi usiku.

Polisi hao wanasemekana kuchukua pesa hizo na kuondoka na gari lao kwa spidi huku wakisahau kofia ya mmoja wao.

Mchina huyo kwa jina Liz Zhixin alitoa ripoti katika kituo cha polisi cha Muthangari na kumpokeza wakili wake kofia hiyo.

Maafisa kutoka Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) wanachunguza kisa ambapo raia mmoja wa Uchina aliripoti kuibiwa shilingi milioni moja na polisi wa trafiki jijini Nairobi.

Raia huyo wa Uchina kwa jina Liz Zhixin anasema kuwa alisimamishwa na maafisa wawili wa polisi wa trafiki katika barabara ya Othaya Alhamisi usiku akitoka Westlands kuelekea Junction Mall.

Kwa mujibu wa Zhixin, aliposimama mmoja wa maafisa hao wa polisi alifungua mlango wa nyuma wa gari lake aina ya Toyota Land Cruiser alikokuwa ameweka pesa hizo.

Afisa huyo kisha alichukua shilingi milioni moja na kuingia katika gari lao aina ya Fielder kabla ya kuondoka mara moja na kuacha nyuma kofia ya mmoja wa maafisa hao wa trafiki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live