Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tito Magoti na mwenzake wahofia mrundikano wa mahabusu Segerea na maambukizi ya corona

101011 Tito+pic Tito Magoti na mwenzake wahofia mrundikano wa mahabusu Segerea na maambukizi ya corona

Mon, 6 Apr 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ofisa wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHCR), Tito Magoti na mwenzake wamedai licha ya Serikali kupunguza msongamano mahakamani ili kuzuia uwezekano wakusambaa kwa virusi vya corona wanaishi kwa hofu kutokana na mrundikano wa mahabusu ulioko gerezani. Magoti na Theodory Giyani (36) ambaye ni mtaalamu wa Tehama wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji fedha kiasi cha Sh 17 milioni. Washtakiwa hao wameeleza hayo leo Jumatano Aprili Mosi mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Janeth Mtega baada ya Wakili Mwandamizi wa Serikali, Wankyo Saimon kueleza upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Akieleza kwa njia ya video mshtakiwa wa kwanza Magoti alidai wamejawa na hofu sana kutokana na msongamano wa mahabusu waliopo gereza la Segerea "Jambo hili linafanya tuishi kwa hofu, kama Watanzania tumeshaurika katika jitihada za kujikinga na ugonjwa hatari wa corona," ameeleza Magoti. Amesema tangu kesi hiyo imeahirishwa siku 14 zilizopita hawajapata nafasi ya kuwasiliana na wakili wao kujua hali za familia ikiwemo mke, watoto na ndugu hivyo wanahisi kutengwa. "Tunaiomba Mahakama iangalie suala hili, katika jambo hili linatujengea hofu na kusababisha kusahaulika katika nchi yetu,"amesema. Wakili Wankyo amesema tangu kutangazwa kwa ugonjwa wa corona Serikali ilitangaza tahadhari mbalimbali na hakuna mtanzania yeyote aliyebaguliwa. "Hakuna mtu yeyote aliyetengwa, gereza limechukua tahadhari ikiwemo kuzuia kuingia kwa wageni hivyo upo utaratibu waliojiwekea wao," Wakili wa utetezi Fulgence Masawe alidai magereza wanabebeshwa kosa lisilo lao la ucheleweshwaji wa upelelezi na ukosaji wa dhamana ndio umesababaisha washtakiwa kuwepo ndani hadi leo. "Tulitegemea tungeambiwa upelelezi umekamilika na kesi imeanza kusikilizwa ombi letu upande wa mashtaka kuliondoa shauri hili mahakamani ambapo watakuwa na uwezo wa kulirudisha muda wowote,"amesema Wakili Massawe. "Sasa ni mwezi wa nne hakuna chochote kinachoendelea tunategemea upande wa mashtaka wanaweza kubadili hati ya mashtaka na kuwaondolea mashtaka yasio na dhamana, baada ya upelelezi kukamilika wanaweza kuyaongeza." Baada ya maelezo hayo Hakimu Mtega aliwataka washtakiwa hao kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya virusi vya corona kwa kufuata miongozo iliyotolewa na kuutaka upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 15 mwaka huu itakapotajwa tena.

Chanzo: mwananchi.co.tz