Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tisa mbaroni wakituhumiwa kuchoma nyumba diwani

466907ba72fd5df06dea8f65e84f393f Tisa mbaroni wakituhumiwa kuchoma nyumba diwani

Wed, 18 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

JESHI la Polisi mkoani Pwani linawashikilia watu tisa kwa tuhuma za kuhusika kuchomwa moto nyumba ya aliyekuwa diwani mteule wa kata ya Kikongo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Kibaha, Fatuma Ngozi (48) na kusababisha kifo chake na watu wengine watano.

Hayo yalisemwa mjini Kibaha na Kamanda wa Polisi mkoani humo, Wankyo Nyigesa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juzi na kuwa majina ya watuhumiwa hao yamehifadhiwa ili kutoharibu ushahidi.

Nyigesa alisema tukio hilo lilitokea Novemba 9 mwaka huu saa 7:00 usiku katika Kijiji cha Chekereni Kata ya Kikongo Tarafa ya Mlandizi Halmashauri ya Kibaha Vijijini wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani.

"Nyumba iliyochomwa moto alikuwa akiishi hapo na alikuwa na familia yake ya watoto sita siku ya tukio hilo na kusababisha vifo hivyo vya watu watano na kufanya watu waliokufa kuwa sita,"alisema Nyigesa.

Baada ya tukio hilo kutokea jeshi la polisi limefanya uchuguzi wa tukio hilo na kufanikiwa kuwakata watuhumiwa tisa, kati yao wanaume wanane na mwanamke mmoja.

"Watuhumiwa wote hawa tumewakamata kutokana na taarifa mbalimbali na ushahidi tuliokusanya dhidi yao na wamehojiwa wote na tunatarajia kuwafikisha mahakamani haraka iwezekanavyo kwa hatua zaidi za kisheria,"alisema.

Aidha alisema kuwa kwa kuwa wanaendelea na upelelezi wa tukio hilo wanahifadhi majina, nyadhifa na kazi za watuhumiwa hao kwa sababu bado wanaendelea kufuatilia na kuwakamata watuhumiwa wengine kwa kadri watakavyoendelea na upelelezi wa tukio hilo.

Chanzo: habarileo.co.tz