Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tisa mbaroni kwa kulima bangi katika eneo la Hifadhi, Shamba lateketezwa

Shamba La Bangi Nyang'wale Tisa mbaroni kwa kulima bangi katika eneo la Hifadhi

Mon, 6 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu tisa Wilayani Nyang’hwale mkoani Geita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kulima bangi katika eneo la msitu wa Hifadhi ya Mienze iliyopo kijiji cha Wavu kata ya Shabaka wilayani humo.

Watu hao wamekamatwa kufuatia Operesheni inayofanywa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na idara ya misitu ambapo tayari mashamba yenye hekari zaidi ya sita yaliyolimwa bangi yameteketezwa.

Akizungumza wakati wa uteketezwaji wa mihadarati hiyo Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale Bi.Grace Kingalame amesema hayupo tayari kuona baadhi ya watu wakifanya biashara ya kulima bangi wilayani humo na kuwataka wenye tabia hiyo kuacha mara moja.

Watu hao wamekamatwa kufuatia operesheni inayofanywa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo Grace Kingalame kwa kushirikiana na jeshi la polisi pamoja na idara ya misitu ambapo tayari mashamba yenye hekari zaidi ya sita yaliyolimwa bangi yameteketezwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live