Wawakilishi wa ngazi za juu wa serikali ya Afrika Kusini watasafiri kuja Tanzania kufuatia kukamatwa kwa mfungwa Thabo Bester aliyetoroka gerezani wakati akitumikia kifungo cha maisha nchini Afrika Kusini.
Thabo Bester na washirika wake wawili walikamatwa na maafisa usalama wa Tanzania Aprili 8 jijini Arusha kufuatia uwepo kwa hati ya kukamatwa kwake baada ya kutoroka gerezani.
Kwa mujibu wa kipindi cha televisheni cha #TheAgenda kinachorushwa na shirika la utangazaji la Afrika Kusini, SABC wawakilishi hao watakuja kuwachukua Thabo Bester na washirika wake wawili, Dkt. Nandipha Magudumana na raia wa Msumbiji Zakaria Alberto.