Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tayari Mbowe na wenzake wamefikishwa Mahakamani

Mbowe 11?fit=680%2C328&ssl=1 Freeman Aikael Mbowe, Mwenyeketi wa CHADEMA

Wed, 15 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu wamefikishwa katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Mbowe na wenzake wamefikishwa mahakamani hapo leo Jumatano Septemba 15, 2021 kwa ajili ya kusikiliza kesi yao.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine ni Halfan Bwire Hassan, Adamu Hassan Kasekwa, na Mohamed Abdillahi Ling'wenya.

Serikali inawasilishwa na jopo la mawakili nane wakiongozwa na wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando, huku washtakiwa wakitetewa na jopo la mawakili 14, likiongozwa na wakili Peter Kibatala.

Kesi hiyo inasikilizwa na Jaji Yusuph Siyani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live