Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tatizo la ndoa chanzo cha mwanamke kuuawa-Madai

67678 Pic+ndoa

Mon, 22 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Imeelezwa kuwa kabla ya Naomi Marijani kuuawa, hakuwa na maelewano mazuri na mumewe.

Mwanamke huyo alitoweka nyumbani kwake Mei 15, 2019  na siku 63 baadaye Jeshi la Polisi nchini Tanzania lilidai kuwa mume wake aitwaye, Khamis Luwongo alikiri kumuua na baadaye kumchoma moto kisha kufukia majivu yake.

Luwongo anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mkewe wakati uchunguzi ukiendelea.

Soma zaidi: VIDEO: Eneo linalodaiwa kufukiwa mabaki ya mwili wa Naomi Marijani

Akizungumza na Mwananchi, Frank Mdong’ola, mjumbe wa serikali ya mtaa wa Kizani, ambako wanandoa hao walikuwa wakiishi alisema alipata taarifa ya wawili hao kutokuwa na uhusiano mzuri kutoka kwa Luwongo.

“Siku ambayo alikuja ofisini kutoa taarifa kwamba mkewe ametoroka na kumuacha mtoto, tulimuuliza imekuwaje hadi mke anaondoka asimuage? Akasema kwa muda mrefu hawakuwa na maelewano,” amesema Mdong’ola.

Pia Soma

Soma zaidi: Anayedaiwa kumuua mkewe, kumchoma moto ashikiliwa polisi

Kwa habari zaidi soma gazeti la Mwananchi la leo Jumapili Julai 21, 2019

Chanzo: mwananchi.co.tz