Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tapeli anavyompa taabu sana Muroto

28731 Pic+muroto TanzaniaWeb

Mon, 26 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Polisi wanamshikilia mkazi wa kijiji cha Malimbika wilayani Gairo, Mkoa wa Morogoro kwa tuhuma ya kujifanya daktari wa binadamu kwa mara ya pili.

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Gilles Muroto alieza jana kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 20 saa 9:30 alasiri kijiji cha Mwakisabe Wilaya ya Chemba mkoani hapa.

Muroto alisema mtuhumiwa alikutwa akitoa huduma ya kitibabu katika jengo lisilo rasmi ambalo linalomilikiwa na Kisusa Iberi, ambako walikuta watu 14 wakihudumiwa mmoja kati yao, akisubiria upasuaji wa uvimbe kwenye paji la uso. Alisema mtuhumiwa alikuwa anatafutwa baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa kama hilo katika mahakama ya Wilaya ya Kongwa.



Chanzo: mwananchi.co.tz