Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yawakamata wahamiaji haramu 65 raia wa Ethiopia

Tanzania Yawakamata Wahamiaji Haramu 65 Raia Wa Ethiopia Tanzania yawakamata wahamiaji haramu 65 raia wa Ethiopia

Tue, 15 Aug 2023 Chanzo: Bbc

Idara ya Uhamiaji imewakamata wahamiaji haramu 65 raia wa Ethiopia ambao walikuwa wanasafirishwa kwa gari ya kubebea mafuta.

Wahamiaji hao walikuwa wanasafirishwa kutoka mkoani Mwanza kuelekea Tunduma.

Walikamatwa Jumatatu majira ya mchana katika kizuizi kilichopo katika kijiji cha Kamsisi Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi.

Idara ya uhamiaji imesema kuwa pia watu 4 raia wa Tanzania walikamatwa akiwemo dereva wa gari hilo.

Watu wote hao wanashikiliwa Kwa hatua zaidi za kisheria.

Mara kwa mara Tanzania hutumika kama njia ya kupita ya wahamiaji haramu kutoka Eritrea na Ethiopia ambao wengi wao huelekea Afrika Kusini au Ulaya. Kwa wale wanaoshindwa kufanikiwa safari yao huishia kukamatwa, wengine hutelekezwa na madereva wakiwa wamekufa au kuwa na hali mbaya kiafya.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM), linakadiria kuwa tangu mwaka 2014 karibu wahamiaji 50,000 wamekufa au kutoweka wakijaribu kufika nchi kama Marekani au Umoja wa Ulaya. Shirika hilo linaamini kwamba idadi halisi ya watu wanaokufa au kutoweka huenda ikawa juu zaidi.

Chanzo: Bbc