Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yaongoza kwa kesi Mahakama ya Afrika

Hukumu Pc Data Tanzania yaongoza kwa kesi Mahakama ya Afrika

Thu, 15 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Jaji Imani Aboud amesema mahakama hiyo imepiga hatua ya kiutendaji ambayo maamuzi yake yamekuwa yakitumiwa na nchi wananchama wa Umoja wa Afrika kubadili mifumo yake ya haki za binadamu.

Pia ameitaja Tanzania kuwa ni nchi inayotumia ipasavyo mahakama hiyo kutokana na zaidi ya asilimia 50 ya kesi zilizoamuliwa kutoka nchini humo. Aliyasema hayo jijini hapa wakati wa kikao cha faragha kilichowakutanisha majaji wa nchi za Umoja wa Afrika chenye lengo la kutathimini utendaji kazi wa mahakama hiyo katika mashauri mbalimbali.

Alisema kwa sasa nchi 34 kati ya 55 wanachama wa Umoja wa Afrika zimeridhia mkataba ulioanzisha kuwa maamuzi ya msingi yaliyoletwa na mahakama hiyo yamefuatwa na nchi wanachama wa umoja huo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live