Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tani 2.4 za Cocaine zakamatwa zilivuka mpaka

Cocaine Yt.jpeg Tani 2.4 za Cocaine zakamatwa zilivuka mpaka

Sun, 5 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi nchini Australia wamefanikiwa kuzuia dawa za kulevya aina ya Cocaine zenye thamani ya takribani dola za Australia bilioni 1 zilizokuwa zinaingizwa Magharibi mwa nchi hiyo.

Tani 2.4 za Cocaine zinazosadikiwa kutokea Mexico zilikamatwa na maafisa wa Australia wakishirikiana na Wamarekani.

Hatua hii inatajwa kuwa kubwa kuwahi kutokea katika vita dhidi ya dawa za kulevya nchini Australia.

Operesheni hiyo ambayo imekuwa ikiendelea tangu Novemba mwaka jana imefanikiwa pia kuwakamata wadau 12 wa dawa za kulevya.

Mnamo Desemba 28 Polisi wa Australia walitumia Cocaine feki iliyofungwa sawa kabisa na mzigo uliokuwa na Cocaine ya ukweli ili kuwakamata wahusika.

Waliuacha mzigo huo takribani maili 40 Magharibi mwa Perth na wakaendelea kuufuatilia kwa kutumia helikopta na drones.

Wahusika walitumia Boti kwenda kuuchukua mzigo huo ndipo watatu kati yao walipokamatwa Desemba 30 wakiwa na tani 1.2 za Cocaine hiyo feki. Watu wengine 9 walikamatwa baadae.

Kaimu Kamishna wa Polisi Tony Longhorn amesema kuwa ” hii imetuongezea kujiamini, kila tunapofanya operesheni hizi tunajipima uwezo wetu.

Utekelezaji wa mikakati shirikishi na ubunifu katika intelijensia ya Polisi itakuwa ufunguo wa kukabiliana na vita dhidi ya dawa za kulevya huko mbeleni”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live