Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tamaa za mapenzi zaongoza makosa ya uhalifu

MASAUNI Tamaa za mapenzi zaongoza makosa ya uhalifu

Mon, 29 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tamaa ya mapenzi inatajwa kuchochea ongezeko la makosa dhidi ya binadamu, maadili ya jamii kwa kwa watu kujichukulia sheria mkononi,kutokana na wivu wa mapenzi, imani za kishirikina, migogoro ya ardhi na mirathi na mmomonyoko wa maadili.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni wakati akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2023/2024 Bungeni mjini Dodoma leo (Mei 29, 2023)

Masauni amefafanua kuwa katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Mei, 2023 makosa makubwa ya jinai yaliyotolewa taarifa katika Vituo vya Polisi yalikuwa 45,455 ikilinganishwa na makosa 43,771 yaliyotolewa taarifa katika kipindi kama hicho 25 mwaka 2021/22. Hili ni ongezeko la makosa 1,684.

Hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ni kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu kuzingatia sheria, kuhamasisha jamii kutoa taarifa za makosa hayo kwa wakati kwa kushirikisha Viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji na kushirikisha Viongozi wa Dini katika kutoa elimu ya maadili mema kwa jamii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live