Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru yawatia mbaroni wafanyabiashara 10 Kariakoo

26307 Pic+takukuru

Sat, 10 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) inawahoji wafanyabiashara 10 wanaotuhumiwa kufanya udanganyifu katika biashara na kuinyima Serikali kodi stahili inayostahili.

Hatua hiyo imechukuliwa ikiwa ni takribani wiki mbili tangu taasisi hiyo itoe tahadhari kwa wafanyabiashara kuhusu udanganyifu huo na mamlaka hiyo kutangaza kulivalia njuga suala hilo.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Novemba 9, 2018 amesema wafanyabiashara hao wanaohojiwa ni kati ya 64 ambao majina yao yanaendelea kufuatiliwa baada kubainika kushiriki kwenye uvunjifu huo wa sheria.

Amesema baada ya Takukuru kutoa tahadhari hiyo maofisa wake walipita kwenye maduka kwa ajili ya kutoa elimu na kuchunguza wafanyabiashara wanaokwepa kodi kwa makusudi.

Katika uchunguzi huo imebainika udanganyifu huo unafanyika kwa aina 10 tofauti ikiwemo wafanyabiashara kutoa risiti zenye kiasi tofauti cha pesa halisi iliyotolewa, kutolewa kwa risiti za kutembelea, kutotolewa kwa risiti za kielektroniki, kutolewa risiti za kughushi na nyinginezo.

Chanzo: mwananchi.co.tz