Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru yawasimamisha kazi vigogo wawili Tanga

99754 Pic+takukuru Takukuru yawasimamisha kazi vigogo wawili Tanga

Fri, 20 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) nchini Tanzania imewasimamisha kazi watumishi wawili wa taasisi hiyo kupisha uchunguzi dhidi yao.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Ijumaa Machi 20, 2020 na kaimu mkurugenzi wa taasisi hiyo, Brigedia Jenerali John Mbungo imewataja watumishi waliosimamishwa ni mkuu wa Takukuru mkoa wa Tanga, Christopher Mariba na ofisa uchunguzi mkuu wa Takukuru mkoa wa Tanaga, Hilton Njau.

Taarifa hiyo imesema watumishi hao wamesimamishwa kutokana na kuhusishwa na tuhuma za kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa mmoja wa watuhumiwa waliokuwa wakichunguzwa.

Kutokana na kusimamishwa kazi kwa Mariba, Dk Sharifa Bungala ameteuliwa kukaimu nafasi hiyo

“Wakati uchunguzi huu ukiendelea,  nimemteua   Dk  Sharifa  Bungala kukaimu nafasi ya Mkuu wa Takukuru mkoa wa Tanga kuanzia leo Machi 20,2020,” imesema taarifa hiyo

Chanzo: mwananchi.co.tz