Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru yawashikilia walimu, wanafunzi VETA kwa rushwa

4715c899895b7c136a5a2da9e236697d Takukuru yawashikilia walimu, wanafunzi VETA kwa rushwa

Wed, 16 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Kagera inawashikilia wanafunzi 38 wa chuo cha VETA Kagera na wakufunzi wao wawili, Francis Mwangosi na Ssenabulya Daud pamoja pamoja na Mkuu wa Chuo hicho, Baluhi Mitinje kwa tuhuma za udanganyifu na rushwa kwenye chumba cha mtihani.

Aidha, taasisi hiyo pia inawashikilia wanafunzi 21 wa Chuo cha Tuinuane VTC na wakufunzi wao wawili, Charles Byabachwezi na Verdiana Myaka pamoja na Mkuu wa chuo hicho Emmanuel Jonas kwa tuhuma za kufanya udanganyifu katika mitihani na matumizi mabaya ya ofisi kinyume na sheria.

Mkuu wa Takukuru mkoani Kagera, John Joseph amesema kuwa wanawashikilia wanafunzi hao pamoja na walimu wao kwa ajili ya

uchunguzi zaidi kabla ya hatua zaidi za kisheria kuchukuliwa dhidi ya wahusika hao.

Sambamba na hilo, Mkuu huyo amesema kuwa wamekamata simu 38 zilizotumiwa na wanafunzi ndani ya vyumba vya mitihani wiki iliyopita pamoja na Sh 151,000/= zilizochangwa na wanafunzi kwenye mchakato wa kuwapatia wasimizi wa mitihani wa taifa wa elimu ya ufundi.

Chanzo: habarileo.co.tz