Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru yawafikisha watatu kortini kwa tuhuma za rushwa

98af5fa646dfd4f76e3391abcfe506de Takukuru yawafikisha watatu kortini kwa tuhuma za rushwa

Mon, 23 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TAASISI ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) mkoani Dodoma imewapandisha kizimbani watu watatu wakituhumiwa kuhusika na vitendo vya kushawishi na kupokea rushwa kinyume cha kifungu namba 15 cha sheria ya Takukuru namba 11 ya mwaka 2007.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo alisema kupandishwa kizimbani kwa watuhumiwa hao ni kutokana jitihada za taasisi hiyo katika kufanya kazi ya kuimarisha utawala bora na kuhakikisha haki inatamalaki katika jamii mkoani humo.

Katika kesi ya kwanza, taasisi hiyo Novemba 13, mwaka huu, ilimpandisha kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma Ofisa Uhamiaji Elibariki Mnghani (29) mkazi wa jijini hapo na kumfungulia mashataka mawili ya kushawishi na kupokea rushwa ya Sh 500,000.

Uchunguzi wa Takukuru ulibaini kwamba saa 5.00 usiku wa Novemba 12, mwaka huu katika eneo la Dodoma Hoteli jijini hapo, mshtakiwa alishawishi na kupokea rushwa ya kiasi hicho cha fedha kutoka kwa Saurabh Tanwar.

Anatuhumiwa kupokea fedha hizo ili kishawishi ili asaidie kuachiwa huru kwa Gangeswaran Thangadurai raia wa India, ambaye alikuwa anashikiliwa na maofisa uhamiaji wenzake kwa kosa la kuwazuia kufanya kazi yao.

Katika kesi ya pili, Takukuru ilimpandisha kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Dodoma fundi magari wa Kampuni ya Yapi Markezi Hamisi Athumani (27) mkazi wa Jiji la Dodoma kumfungulia mashataka sita ya kushawishi na kupokea rushwa ya Sh 300,000 kutoka kwa wananchi watatu.

Uchunguzi wa taasisi hiyo ulibaini kwamba kati ya Oktoba mwaka jana na Januari mwaka huu, mshtakiwa alipokea fedha hizo ili awasaidie wananchi hao kupata ajira katika kampuni hiyo anayofanyia kazi.

Katika kesi ya tatu, taasisi hiyo imemfikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Kongwa, Ofisa Afya Mkuu Msaizidi wa Mamlaka ya Mji Mdogo Kibaigwa wilayani Kongowa, Anania Madono (57) na kumfungulia mashtaka mawili ya kushawishi rushwa ya Sh 200,000 na na akapokea Sh 160,000 kinyume cha sheria ya Takukuru.

Uchunguzi wa Takukuru umebaini kwamba mwanzoni mwa mwezi huu, mshatakiwa alikamata na kushikilia madumu 63 yenye lita 309 za mafuta ya alizeti mali ya mtoaji taarifa hiyo kwa madai kwamba hayana taarifa za vifungashio na alimtaka amlipe fedha hiyo ili ayaachie madumu hayo.

Novemba 8, mwaka huu, taasisi hiyo imekamata mtuhumiwa katika eneo la Kibaigwa wilayani Kongwa baada ya kupokea rushwa na kumrejeshea mtoa taarifa hizo madumu yake ya mafuta aliyokuwa ameyashikilia ofisini kwake.

Chanzo: habarileo.co.tz