Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru yawafikisha mahakamani Wachina kwa kughushi

82471 Takukuru+pic Takukuru yawafikisha mahakamani Wachina kwa kughushi

Fri, 1 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imewafikisha mahakamani wafanyabiashara watatu wa mafuta kwa kughushi na kufanya kazi Tanzania bila kuwa na kibali.

Wafanyabiashara hao ni raia wawili wa China, Yu Hattao na Zhang Zhi Xin ambao ni wamiliki wa kampuni ya Shin Up Limited iliyopo Visiga wilaya ya Kibaha mkoani Pwani na John Mnyele.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Oktoba 31, 2019 kaimu mkurugenzi wa Takukuru,  Ali Mfuru amesema taasisi hiyo kwa kushirikiana na  polisi wamewafikisha mahakamani watu hao kwa makosa tofauti.

“Mshtakiwa wa kwanza Yu Hattao anakabiliwa na makosa mawili la kughushi kinyume na kifungu cha 333, 335 (a) na 337 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 (marejeo ya 2002) huku akikabiliwa na kosa la kufanya kazi nchini bila kibali kinyume na kifungu cha 9 (1) (a) (b) na 20 (d) cha kanuni za ajira na 1 ya mwaka 2015,” amesema Mfuru.

Amesema makosa mengine yanayowahusu  watuhumiwa wote ni kuendesha shughuli za ujenzi bila kupata kibali cha ukaguzi wa mazingira kinyume na kifungu cha 81 cha sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake za mwaka 2005 na kifungu cha 60 (1) vikisomwa kwa pamoja na kifungu namba 191 cha sheria ya mazingira.

“Kosa jingine ni kujenga mtambo wa kusafisha mafuta ya dizeli bila kibali cha Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) kinyume na kifungu cha 127 (1) na (2) cha sheria ya Petroli Na 21 ya mwaka 2015,” amesema Mfuru.

Chanzo: mwananchi.co.tz