Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru yawadaka viongozi wa vijiji kwa rushwa 70,000

PCCB DOM Takukuru yawadaka viongozi wa vijiji kwa rushwa 70,000

Thu, 7 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Dodoma imefanikiwa kumfikisha Mahakamani Afisa Mtendaji wa kijiji cha Muungano wilayani Chamwino mkoani humo pamoja na Mwenyekiti wa kijiji hicho baada ya kupokea rushwa ya Shilingi 70, 000.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo, amesema viongozi hao wamefikishwa Mahakamani kwa Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Dodoma.

Aidha, mbali na kuwafiksha Mahakamani watu hao, pia Takukuru Dodoma imefanikiwa kuokoa Shilingi milion 194 kutoka katika vyama sita vya Ushirika na wanatarajia kuzirejesha katika vyama husika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live