Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru yawadaka saba tuhuma za rushwa, wamo walimu wawili

68782 Pic+takukuru

Mon, 29 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Dodoma, nchini Tanzania, inawashikilia watu saba kwa makosa ya kuomba na kupokea rushwa kinyume na kifungu cha 15 (1).

Miongoni mwa waliokamatwa ni walimu wawili wa shule ya Sekondari Viwandani kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya Sh20,000 ili kutoa cheti kwa mwanafunzi huku mmoja akinaswa kwa rushwa ya Sh1.2 milioni kwa kosa na kumhonga Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Patrobasi Katambi.

Mkuu wa Takukuru mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo akitoa taarifa hiyo leo Jumatatu Julai 29,2019 kwa waandishi wa habari amesema watu hao wanatarajia kupelekwa mahakamani wakati wowote kuanzia leo ili kujibu tuhuma hizo.

Kibwengo amewataja wanaopelekwa mahakamani ni Nahid Bahadur Hirji (33) ambaye alitaka kumpa fedha Mkuu wa Wilaya, Katambi ili asifuatilie upungufu wa baraza la nyumba la wilaya kuhusu hukumu ya kesi iliyokuwa mbele yao kati ya mtuhumiwa na dada yake.

Wengine ni Omary Mtauka ambaye ni msaidizi wa ofisa mtendaji kata ya Makutupora, kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya Sh110,000 kwa mzee wa miaka 78, John Matambi (34) ambaye ni mtendaji wa kijiji cha Matumbulu kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya sh 65,000.

Wengine ni Venance Mayo na Sulaith Rusheke ambao ni walimu wa shule ya Viwanda iliyoko katikati ya Jiji la Dodoma wakipokea Sh20,000 ili watoe living certificate na mwingine ni mtumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA) Abdulhakim Kabunga (26) ambaye alipokea Sh30,000 ili kumsaidia mtu kupata kitambulisho kwa haraka zaidi.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz