Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru yataka neno toka CCM makao makuu

1a827b762acdab3845a83c0d39527cea Takukuru yataka neno toka CCM makao makuu

Mon, 3 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoa wa Rukwa umekiandikia barua Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupata tafsiri ya picha zinazoendelea kuzagaa mtandaoni zikimuonesha Naibu Waziri Ofi si ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Josephat Kandege akigawa fedha kwa wajumbe hadharani akiwa amevaa sare za chama chake na akichezewa ngoma.

Kandege ambaye alikuwa mbunge wa Jimbo la Kalambo ametia nia ya kutetea nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao ambapo katika kura za maoni aliibuka kidedea.

Aidha taasisi hiyo imekiri kumhoji aliyekuwa mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Rukwa, Bupe Mwakangata kuhusiana na kujihusisha na matukio yanayoashiria harufu ya rushwa kabla ya kuanza kwa mchakato wa kura za maoni.

Mwakangata ametia ni ya kugombea ubunge viti maalumu mkoa wa Rukwa ambaye aliibuka kidedea katika kura za maoni zilizofanyika hivi karibuni.

Akizungumzia picha za mtandaoni Kamanda wa Takukuru mkoa wa Rukwa, Hamza Mwenda alikiri kuiona picha ya Kandege mtandaoni mwezi mmoja uliopita ikimuonesha akigawa fedha hadharani kwa watu wanaodhaniwa kuwa wajumbe .

“Baada ya kufanya uchunguzi wetu tumebaini kuwa ‘clip’ hiyo ya video inaonesha kuwa tukio hilo la Kadege kugawa fedha kwa wananchi hadharani huku akichezewa ngoma lilifanyika Julai 7 mwaka 2018 ikiwa ni miaka mitatu baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2015... tunashirikiana na mamlaka zingine katika uchunguzi wetu ili kubaini tarehe halisi lilipofanyika tukio hilo na kumpata aliyesambaza mitandaoni... Lakini pia tumeandika barua na kuiwasilisha CCM tukiomba kupewa tafsiri sahihi ya tukio hili,”alieleza.

“Nimepigiwa simu nyingi sana kutoka Dar es Salaam na Dodoma kuhusiana na picha hii iliyosambaza mtandaoni “ alieleza Kuhusu tuhuma za Bupe Mwakang’ata alikiri kuwa alilalamikiwa kujihusisha na rushwa mapema haya kabla ya kuanza kwa mchakato wenyewe wa kura za maoni.

“Ni kweli maofisa wa Takukuru walikwenda katika eneo la tukio na kukuta wajumbe wa Umoja wa Wanawake (UWT) wa CCM wakiwa na fulana mpya, walikiri kupewa na Mwakang’ata lakini aliondoka eneo hilo muda mfupi baadaye kwamba walikuwa wakizungumzia mambo yao ya chama,”alieleza Mwenda

Chanzo: habarileo.co.tz