Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru yashikilia wanafunzi 13 wa IRDP kwa rushwa

F5670f9c684a2049c67e1d53e26224b4 Takukuru yashikilia wanafunzi 13 wa IRDP kwa rushwa

Sun, 17 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Dodoma inawashikilia wanafunzi 13 wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa na udanganyifu wa mitihani ya marudio.

Akitoa taarifa ya utendaji wa taasisi ya robo ya tatu ya mwaka, kuanzia Oktoba hadi Desemba mwaka huu, mkuu wa Takukuru mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo alisema wanafunzi hao wa mwaka wa tatu 2020 wanashikiliwa kwa kufanya udanganyifu katika mtihani wa marudio somo la Applied Statistics II uliyofanyika Novemba mwaka jana kwa mwaka wa tatu.

Uchunguzi wa awali uliofanywa na taasisi hiyo unaonesha kwamba wanafunzi hao walitumia rushwa kupata mitihani hiyo ili warudie nje ya chumba cha mitihani karibu na chuo hicho.

Baada ya kufanya mitihani hiyo nje ya chumba cha mitihani karibu na chuo hicho, wanafunzi hao walijaribu kuingiza katika mfumo rasmi karatasi za matokeo walizotumia kujibia mitihani hiyo ndipo chuo kikabaini ujanja huo na kuripoti Takukuru.

"Wanafunzi hao walitaka kuingiza makaratasi ya mitihani hiyo kwenye mfumo rasmi wa matokeo ya chuo kwa kuchomoa karatasi walizofanya kwanza, ndipo chuo kikabaini na kuripoti Takukuru," alisema Kibwengo.

Kibwengo alisema, kutokana na tuhuma hizo wanazokabiliwa nazo wanafunzi hao, Takukuru inawatafuta waliomaliza masomo yao miaka ya nyuma lakini wapo mazingira nje ya chuo. Aliwataja wanafunzi wawili kuwa wanaonekana ndio viunganishi wa mbinu hizo.

Alisema wanafunzi hao wanatakiwa kuripoti mara moja katika ofisi za Takukuru mkoani Dodoma kwa ajili ya kusaidia uchunguzi wa nani alitoa mitihani chuoni hapo kwa wanafunzi hao.

Alisema Takukuru inaendelea na uchunguzi kubaini mitihani hiyo waliipataje na kama kuna walimu wanahusika na mbinu hizo.

Alisema uchunguzi ukikamilika Takukuru itawafikisha mahakani wahusika wote katika sakata hilo la kufanya udanganyifu katika mitihani vyuoni.

Vile vile, katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Oktoba hadi Desemba mwaka jana, Takukuru ilipokea malalamiko 178 ya rushwa na makosa yanayohusiana na hayo.

Serikali za mitaa zinaongoza kwa kuwa na malalamiko asilimia 23, mikopo umiza na sekta binafsi asilimia 20, ardhi asilimia 14, vyama vya siasa na uchaguzi asilimia sita na afya yote asilimia sita.

Katika kipindi hicho, Takukuru imefanya uchunguzi wa majalada 16 na kukamilisha. Pia mashauri 13 yamefunguliwa mahakamani. Aidha, mahakama ilitoa uamuzi katika mashauri 12 ambayo jamhuri imeshinda 10 na kushindwa mawili.

Chanzo: habarileo.co.tz