Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru yaomba kwenda gerezani kumhoji mshtakiwa

38262 Takukurupic Takukuru yaomba kwenda gerezani kumhoji mshtakiwa

Fri, 25 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imeiomba mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kwenda gerezani kumhoji mshtakiwa wa pili Alloycious Mandago katika kesi ya kuisababishia Serikali hasara ya Sh2bilioni.

Wakili wa Takukuru Leonard Swai ameeleza hayo leo Alhamisi, Januari 24, 2018 mbele ya hakimu mkazi mkuu Thomasi Simba wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Swai amedai kesi hiyo iko hatua za mwisho kwa ajili ya kuandaa maelezo lakini wanaombi kwa ajili ya kumhoji mshtakiwa wa pili akiwa magereza.

"Kesi imekuja kwa ajili ya kutajwa tuko hatua za mwisho kwa ajili ya kuandaa maelezo lakini tunaombi kwa ajili ya kumhoji mtuhumiwa wa pili gerezani," alidai Wakili Swai.

Mahakama imeridhia mshtakiwa huyo kuhojiwa na kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 8, mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

Mbali na Mandago, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni mfanyabiashara Mohamed Yusufali na Isaac Kasanga ambao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 39 likiwemo la kuisababishia serikali hasara ya Sh2 bilioni.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Machi 2, 2010 na Aprili 26,2016 katika maeneo tofauti ndani ya jiji la Dar es salaam walikula njama kwa kughushi, kukwepa kulipa kodi na kutakatisha fedha.

Katika shtaka la pili linalomkabili mshtakiwa wa tatu Kasaga anadaiwa, katika ofisi za Wakala wa Usajili (Brela) zilizoko manispaa ya Ilala aliwasilisha nyaraka ya uongo yenye fomu namba 128 ya Mei 2, 2016 akionyesha kuwa Machi 4, 2012 wakurugenzi wa kampuni ya Superior Financing Solution Limited ni Mohamed Mustafa Yusufali, Izack Kassanga na Maria Barnett.

Katika shtaka lingine la utakatishaji fedha kinyume na sheria linalowakabili washtakiwa wote, inadaiwa kati ya Marchi 4, 2011 na 13 Aprili 2016 katika maeneo tofauti ndani ya mkoa wa Dar es salaam akiwa mmiliki na Mkurugenzi wa kampuni ya Superior Financing Solution Limited walijihusisha na muamala wa kiasi cha Sh2.9 bilioni wakijua fedha hizo zinatokana na zao la pesa haramu.

 

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz