Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru yaokoa rushwa ya Sh70bilioni

31083 Takukurupic TanzaniaWeb

Wed, 12 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imesema katika kipindi cha mwaka mmoja imeokoa Sh70.3bilioni zilizokuwa ziingie mifukoni mwa wala rushwa.

Kati ya kiasi hicho, Sh45bilioni zilikuwa zimeelekezwa katika miradi mikubwa ya maji.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru,  Diwani Athuman leo Jumanne Desemba 11, 2018 mjini Dodoma katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa makamanda wa taasisi hiyo wa mikoa na maofisa wake mbalimbali.

Athuman amesema mapambano dhidi ya rushwa bado ni vita kubwa inayohitaji ujasiri na uzalendo na ushirikiano.

Amesema katika kipindi cha mwaka mmoja kesi 495 zimefunguliwa na nyingi zikiwa ni kesi na kwamba nyingi walishinda tofauti na zamani.

Diwani amesema katika uongozi wake wa miezi mitatu ndnai ya taasisi hiyo amebadili mfumo wa utendaji na mtazamo, kwmaba anashirikiana na wenzake kuwapeleka watu mahakamani bila kuzingatia ukubwa wala mwonekano wa nafasi zao.

Ametoa mfano jinsi watumishi wa kiwanda cha chai mkoani Tanga, na makandarasi waliokuwa wakisimamia mradi wa maji wa Ntomoko mkoani Dodoma jinsi walivyofikishwa mahakamani.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz