Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru yaokoa bilioni 1.2/- Moi, 23 kitanzini kwa ubadhilifu

88c67cc3e645dbd40e87c4f580d8b658 Takukuru yaokoa bilioni 1.2/- Moi, 23 kitanzini kwa ubadhilifu

Thu, 14 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru), kwa kushirikiana na Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), wamefanikiwa kudhibiti uchepushaji na ubadhirifu wa dawa za thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 1.2 uliokuwa unafanywa na wa watumishi wa kitengo cha famasia katika taasisi hiyo.

Aidha, katika sakata hilo, wafamasia 23 wa MOI, wanahojiwa ambapo baadhi yao baada ya kubaini wanachunguzwa, walikiri kufanya ubadhirifu huo na kuomba Takukuru iwakubalie warejesha fedha.

Akizungumzia tukio hilo leo, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru,John Mbungo amesema fedha hizo zilikuwa zinachepushwa katika mfumo wa MEDPRO4 ambao ni wa kutunza taarifa za kumbukumbu za utoaji wa dawa na vifaa tiba kwa wagonjwa unaotumiwa na MOI

Chanzo: habarileo.co.tz