Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru yamshikilia mkurugenzi kampuni ya OBC

43728 Pic+takukuru Askofu aishauri Serikali kuhusu uharibifu wa mazingira

Tue, 26 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) inamshikilia mkurugenzi wa kampuni ya wawekezaji kutoka Falme za Kiarabu ya Ortello Business Cooperation (OBC), Isack Lesion Mollel kwa uchunguzi.

Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Arusha, Frida Wikes alitoa taarifa hiyo leo Jumatatu Februari 25, 2019 kwa vyombo vya habari na kueleza kuwa uchunguzi wa tuhuma zake ambazo hata hivyo hazikutajwa unaendelea.

"Tumekuwa tukipokea maswali kutoka kwa waandishi juu ya kumshikilia Mollel kwa taarifa hii tunathibitisha ni kweli Takukuru mkoani Arusha inamshikilia mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Ortello Business Corporation Limited (OBC) Mollel kufuatilia uchunguzi unaoendelea dhidi yake," imeeleza taarifa hiyo.

Mkurugenzi huyo anashikiliwa siku chache baada ya kufikishwa mahakamani, akikabiliwa na makosa 10 ya kuwapa kazi raia wa kigeni 10 katika kambi za kampuni hiyo Loliondo kinyume cha sheria.

Wafanyakazi hao ambao wapo nje kwa dhamana baada ya kufikishwa mahakamani wiki iliyopita, walikuwa wakifanyakazi ya kuandaa mapokezi ya Mfalme wa Dubai ambaye anatarajiwa kutembelea nchini hivi karibuni.



Chanzo: mwananchi.co.tz