Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru yamburuza mwalimu mahakamani

Mon, 20 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mtwara. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  (Takukuru) mkoa wa Mtwara, imemfikishaka katika Mahakama ya Wilaya Masasi aliyekuwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi Masasi, Mwanaidi Mtaka kwa kosa la ubadhirifu.

Mwalimu huyo anatuhumiwa kwa kosa la kutumia nyaraka zenye maelezo ya uongo kumdanganya mwajiri wake kwamba ametumia Sh1.5 milioni kwa matumizi ya ofisi licha ya kuzitumia kwa matumizi binafsi.

Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Mei 17,2019 na kamanda wa Takukuru mkoani Mtwara, Stephene Mafipa imedai kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo mwaka 2015 akiwa mwalimu wa shule ya msingi Masasi wilayani humo.

“Inadaiwa mwalimu huyo alitumia na kuwasilisha stakabadhi zilzoonyesha kuwa alitumia Sh1,578,000 kununua vifaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya shule akijua kwamba hakuvinunua,” imeeleza taarifa hiyo.

Kufuatia tuhuma hizo, kamanda huyo wa Takukuru amesema mtuhumiwa anashitakiwa kwa makosa ya kutumia nyaraka zenye maelezo ya uongo  kumdanganya mwajiri wake kinyume na kifungu cha 22 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Aidha, taarifa hiyo inadai kuwa mtuhumiwa anashtakiwa kwa kosa la ubadhirifu na ufujaji wa mali ya umma kinyume na kifungu cha 28(1) cha sheria ya kuzuia na kupamana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz