Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru yakamata viongozi 52 wa vyama vya ushirika

80653 Pic+takukuru

Fri, 18 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Lindi. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) nchini Tanzania  inawashikilia viongozi 52 wa vyama vya ushirika vya korosho kwa kushindwa kuwalipa wakulima Sh436 milioni.

Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo alisema hayo jana Alhamisi Oktoba 17, 2019 wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Lindi.

Brigedia Jenerali Mbungo alisema wamewakamata viongozi hao ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Tanzania, John Magufuli aliyetaka wahusika wakamatwe ili  wakulima hao walipwe kabla ya msimu mpya wa mauzo haujaanza.

Agizo la Rais Magufuli lilitokana na taarifa iliyotolewa kwake na  Naibu Waziri wa  Kilimo, Husein Bashe wakati alipokuwa akiwahutubia wakazi wa Ruangwa mkoani Lindi katika mkutano wa hadhara na kueleza kuwa wakulima hao wanadai malipo yao.

“Tangu Takukuru ianze kuhakikisha vyama vya msingi vya ushirika (Amcos) zinavyodaiwa na wakulima wa ufuta zinarejeshewa fedha zinazodaiwa, imefanikiwa kurejesha zaidi ya Sh46 milioni.”

“Ninapenda wananchi wote wajue zoezi hili linaendelea na kesho tutakuwa hapa tumeweka kambi hapa kuhakikisha wakulima wanarejeshewa  fedha zao na vyama  vyote ambavyo havitaki kuwalipa wakulima fedha zao,” alisema mkurugenzi huyo.

Pia Soma

Advertisement
Katika hatua nyingine, Takukuru  imesema inawashikilia watumishi wawili wanaotuhumiwa kuandaa nyaraka hewa za Sh200 milioni.

Aliwataja watumishi hao ni Clemence Olomi ambaye ni mhasibu wa hospitali ya Mkoa wa Lindi, Mhandisi Msaidizi wa Halmashauri ya Lindi,  Zebedayo Selemani kwa ubadhirifu wa wodi ya watoto na choo cha wagonjwa na maabara.

“Hawa wanatuhumiwa kuandaa nyaraka za malipo hewa na kufanya malipo yanayozidi kiwango kilichoainishwa katika mikataba iliyoingiwa na wazabuni mbalimbali,” alisema.

Chanzo: mwananchi.co.tz