Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru yaburuza kortini watumishi 5 wa Sikonge

3b4fc4751bf782451cc1cc3760d60765 Takukuru yaburuza kortini watumishi 5 wa Sikonge

Fri, 16 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Tabora imewafi kisha mahakamani watumishi watano wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kujibu mashitaka ya kuomba na kupokea rushwa.

Washitakiwa hao ni watumishi wa Idara ya Maliasili. Walisomewa mashitaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Tabora mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa, Gabriel Ngaije.

Hao ni Ofisa Wanyamapori wa Wilaya, Kelvin Msacky, maofisa misitu wasaidizi Lambert Kombe, Manfred Lyimo na Jovin Sapola na Ofisa Misitu Mkuu Wilaya, Edgar Rwezaula.

Upande wa mashitaka ukiongozwa na mawakili, Simon Mashibgia na Eunice Masalu wa Takukuru Mkoa wa Tabora, waliieleza mahakama hiyo kuwa washitakiwa walitenda kosa hilo Septemba 3, mwaka huu.

Katika kesi hiyo ya jinai Namba 93 ya mwaka 2020, ilidaiwa kwa siku hiyo washitakiwa walikamatwa katika Kijiji cha Lunguya wilayani Sikonge, baada ya kuomba na kupokea rushwa ya Sh milioni 18 kwa mfugaji ng’ombe, Faida Derefa.

Upande wa mashitaka ulidai washitakiwa hao wakiwa ni watumishi wa serikali, waliomba na kupokea kiasi hicho cha fedha ili wawaachie ng’ombe wa Derefa, ambao walikutwa wakichungwa ndani ya msitu wa Hifadhi ya Kijiji cha Kanala.

Washitakiwa walikana mashitaka na walipelekwa rumande, kwani walishindwa kutimiza masharti ya dhamana. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Oktoba 22, mwaka huu wakati shauri hilo litakapoanza usikilizwaji hoja za awali.

Chanzo: habarileo.co.tz