Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru yabaini mbinu mpya ya uibaji madini

61707 TAKUKURU+PIC

Sun, 9 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Bukoba. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) Mkoa wa Kagera imebaini mbinu mpya ya uibaji wa madini ya dhahabu kupitia vilainishi vinavyowezesha kiasi kikubwa kubaki kwenye mchanga wa madini ya dhahabu ‘makinikia’ baada ya uchenjuaji.

Akitoa taarifa ya utendaji wa taasisi hiyo kwa miezi tisa leo Juni 7, 2019, Mkuu wa Taasisi hiyo Mkoa wa Kagera, John Joseph amesema udanganyifu huo kupitia vilainishi kutoka nje umegundulika katika mgodi wa Stamigold Wilayani Biharamulo.

Amesema kupitia vilainishi hivyo kiasi kikubwa hubaki kwenye mchanga baada ya uchenjuaji na mabaki huchukuliwa kwenda kufanyiwa uchenjuaji mpya na kupata kiasi kikubwa cha madini hayo.

"Tumegundua udanganyifu kwa wanaopeleka vilainishi kwa ajili ya kuchenjua dhahabu kwenye mgodi wa Tulawaka (Stamigold), badala ya kupata gramu 100  unapata kumi na wanachukua mabaki kwenda kufanya uchenjuaji mpya," amesema Joseph

Hata hivyo hakutaja kiasi cha dhahabu na thamani yake vinavyokadiriwa kuibiwa kupitia mbinu ya kutumia vilainishi na njia hiyo imekuwa ikitumika kwa takribani miaka miwili sasa na kubainisha taratibu za kisheria zimeanza kuchukuliwa.

Kuhusu miradi ya barabara iliyotelekezwa na wakandarasi katika Manispaa ya Bukoba pamoja na kulipwa sehemu ya fedha, Joseph amesema uchunguzi upo na hatua za mwisho na taarifa itatolewa.

Pia Soma

Ametaja baadhi ya maeneo yenye kero za vitendo vya rushwa kuwa ni pamoja na ardhi, polisi kubambikiza kesi na kuwa taasisi hiyo imefanikiwa kuokoa 7.8 bilioni ambazo zingepotea kupitia miradi mbalimbali.

Chanzo: mwananchi.co.tz