Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru wamdaka mzazi akitoa rushwa ili mtoto wake aliyefaulu asiendelee na masomo

65087 Pic+takukuru

Tue, 2 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Sio rahisi kuamini lakini ndivyo ilivyotekea, mzazi  amekamatwa akitoa rushwa ili mtoto wake aliyefaulu vizuri kidato cha kwanza asiendelee na masomo badala yake abaki nyumbani akichunga mifugo.

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, mkoa wa Arusha nchini Tanzania,  Frida Wikesi anamtaja mzazi huyo leo Jumatatu Juni 1,2019 ni  Victoria Tarmo mkazi wa kata ya Mang'ola wilaya ya Karatu, ambaye hakutaka mtoto wake Paulo Qwande kwenda sekondari licha ya kufaulu.

Mzazi huyo alinaswa akimpa rushwa ofisa mtendaji wa kata ya Mang'ola, Petro Ngarikoi ambaye kabla ya kupokea rushwa hiyo ya Sh20,000 alitoa taarifa Takukuru ambao waliandaa mtego uliozaa matunda na mtuhumiwa amefikishwa mahakamani.

Mtoto huyo tayari amepelekwa shule ya Domeli iliyopo Karatu ambayo alikuwa amefaulu kuanza kidato cha kwanza.

Hili ni kati ya matukio machache tu yaliyoripotiwa ya wazazi wa jamii ya wafugaji, kuhonga maofisa watendaji na wakati mwingine walimu wakuu ili watoto wao waliofaulu shule, wasiendelee na masoko ili wachunge ama kuolewa na kuna wazazi wamekuwa wakihonga hadi ng'ombe.

Chanzo: mwananchi.co.tz