Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru waendelea kuwachunguza Mnyeti, Ole Millya

72145 Mnyetipic

Tue, 20 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Babati. Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Manyara, Fidelis Kalungura amesema wanaendelea na uchunguzi wa madai ya Mkuu wa mkoa huo, Alexander Mnyeti na mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya kutuhumiana rushwa na kutishia wafanyabiashara kwa silaha.

Akizungumza jana Agosti 19, Kalungura amesema bado wanaendelea na uchunguzi wa suala hilo.

"Hatuwezi kuzungumza lolote kwa sasa kwani tunaendelea na uchunguzi wa matukio haya mawili, ila hatutaki kunukuliwa kwenye vyombo vya habari, tutawajulisha tukiwa tayari," amesema.

Mnyeti na Ole Millya walituhumiana hadharani Julai 28, mwaka huu katika Mji mdogo wa Mirerani, mbele ya Waziri wa Madini, Dotto Biteko wakati akipokea taarifa ya kamati ya kutatua migogoro ya wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite na kampuni ya TanzaniteOne.

Awali, Millya alimtuhumu hadharani Mnyeti kuwa anawatetea wawekezaji wakubwa TanzaniteOne kutokana na maslahi yake.

Mnyeti naye alidai Ole Millya analalamikiwa na baadhi ya wafanyabiashara kuwatishia bastola ili wampatie fedha.

Habari zinazohusiana na hii

Baada ya tuhuma hizo kutolewa hadharani, Kalungura aliahidi kuchukua hatua kwa kuanza uchunguzi wa matukio hayo mawili.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz