Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru kuchunguza mwalimu kukatwa mshahara miezi 38

80677 Pic+mwalimu

Fri, 18 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Musoma. Tume ya Utumishi Walimu (TSC) Mara inachunguzwa kwa adhabu ya kumkata mwalimu asilimia 50 ya mshahara wake.

Kutokana na adhabu hiyo, mwalimu huyo alijikuta akikosa mshahara miezi 38.

Akizungumza mjini hapa jana, mkuu wa Takukuru mkoani Mara, Alex Kuhanda alisema wakati mwalimu huyo akiadhibiwa, mwalimu mwingine anayedaiwa kutoonekana kazini zaidi ya siku 200 ameachwa bila adhabu.

Kuhanda alisema iwapo tuhuma za mwalimu huyo kutokuwepo kwa muda huo zingethibitika angetakiwa kulipa Sh70,664 kwa mujibu wa taratibu za utumishi.

Alisema mwalimu huyo alipewa adhabu ya kukatwa asilimia 50 ya mshahara kwa mwaka na ukiongeza makato mengine kwa mujibu wa sheria za utumishi, alijikuta akikosa mshahara kwa miezi 38 na hivyo kukatwa jumla ya Sh9.8 milioni.

Kuhanda alisema tume hiyo pia iliamuru mwalimu huyo aondolewe katika shule ya sekondari aliyokuwa akifundisha na kuhamishiwa shule ya msingi na kutakiwa kujigharamia uhamisho wa kwenda kituo kipya cha kazi.

Pia Soma

Advertisement
“Huyu mwalimu salary slip yake inasoma ziro kwa miezi yote hiyo na amepewa adhabu zaidi ya sita ikiwemo kulazimishwa kutodai mishahara ya miezi 28 kipindi alichosimamishwa wakati shauri lake likisikilizwa na kutotoka nje ya kituo chake bila kibali cha TSC,” alisisitiza Kuhanda an kuongeza kuwa ofisi yake imeanza uchunguzi.

Kwa upande wake, katibu wa TSC Butiama, Mariba Wambura alisema kwa kanuni za TSC, mwalimu asipofika kazini zaidi ya siku 5 anapaswa kupewa adhabu ikiwemo kufukuzwa kazi.

Alisema yeye hana mamlaka kuwajibisha mwalimu yeyote isipokuwa kamati ya tume ya wilaya husika hivyo adhabu iliyotolewa ni kwa mujibu wa taratibu zao na ni baada ya kamati kukutana na mtuhumiwa kuhojiwa.

Wambura alisema hata hivyo kila mwalimu anayepewa adhabu hupewa siku 45 za kukata rufaa kwa hiyo kama mwalimu huyo hakukata rufaa ina maana alikiri makosa yake na hivyo alistahili adhabu hiyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz