Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru: Rushwa ya ngono haikubaliki, tuwaumbue

C91b5519851779817e849d52984b9496 Takukuru: Rushwa ya ngono haikubaliki, tuwaumbue

Wed, 10 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KATIKA kuadhimisha Siku ya Wanawake Dun=iani, Taasisi Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), imewataka wananchi kubadili fi kra kwa kufi chua vitendo vya rushwa ikiwemo rushwa ya ngono.

Katika tamko lake jana kuadhimisha siku hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali, John Mbungo, alisema wakati kaulimbiu ya mwaka huu ya siku hiyo ilikuwa “Wanawake katika uongozi: Chachu kufikia dunia yenye usawa,” yeye na watumishi wake wa Takukuru wanasema, “Badili fikra, rushwa ya ngono haikubaliki, tuwaumbue.

” Alisema Siku ya Wanawake Duniani inalenga kutambua mafanikio ya mwanamke bila kujali rangi, dini, kabila au siasa na kutafakari maendeleo ya mwanamke, hivyo Takukuru inaunga mkono juhudi zinazoendelea duniani za kuhakikisha wanawake wanalindwa dhidi ya unyanyasaji na udhalilishaji wa aina zote ikiwemo kulazimishwa kutoa rushwa ya ngono.

Alisema kwa kutambua kuwa vyuo vikuu ni viwanda vya kuandaa wataalamu wa fani mbalimbali za utoaji huduma, uzalishaji na malezi katika familia, Takukuru ilifanya utafiti katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Februari mwaka jana kwa lengo la kupata taarifa za kisayansi zitakazosaidia kukabiliana na tatizo la rushwa ya ngono katika taasisi za elimu ya juu.

“Matokeo ya utafiti yalibainisha kuwa tatizo la rushwa ya ngono kwenye vyuo tafitiwa lipo, wanafunzi asilimia 58 na watumishi asilimia 69 walieleza kuwepo kwa matukio ya vitendo vya rushwa ya ngono,” alisema Brigedia Jenerali Mbungo.

Alisema sababu kubwa ya kuwepo kwa rushwa ya ngono katika taasisi tafitiwa zinatokana na mifumo dhaifu ya kudhibiti matumizi mabaya ya mamlaka, kusimamia uwajibikaji, mifumo dhaifu ya ajira hasa za wahadhiri, ufinyu wa huduma muhimu kama hosteli, mikopo ya elimu na mmomonyoko wa maadili.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, mbinu zilizobainika kushawishi rushwa ya ngono ni pamoja na kutoa alama za chini kwenye mitihani, vitisho vya kutofaulu kwa wanafunzi, ahadi za ajira, cheo, chumba chuoni, nafasi ya uongozi, kuongeza alama za ufaulu na kusaidia kupata ufadhili wa masomo.

“Nawasihi wananchi kutumia fursa hizi kuwafichua wadhalimu wanaodai rushwa ya ngono na rushwa nyingine ili kwa ushirikiano huo tukomeshe vitendo hivyo,” alisema Brigedia Jenerali Mbungo. Kutokana na hali hiyo, alisema taasisi hiyo inafuatilia utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa baada ya kufanya utafiti katika vyuo vikuu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz