Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tajiri Arusha atishia  kwa bastola, baada ya mahakama kutoa hukumu

6e82e339786555f8513c53293e00cdcd.jpeg Tajiri Arusha atishia  kwa bastola, baada ya mahakama kutoa hukumu

Thu, 20 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Jeshi la polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia wafanyabiashara wawili akiwemo Mfanyabiashara maarufu Jijini Arusha Dk Philemon Mollel maarufu kwa jina la Monaban kwa kosa la kutumia vibaya silaha za moto wanazomiliki baada kutishiana kuuwana kwa risasi juzi katika eneo la kituo cha mafuta cha Ngulelo jijini Arusha.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani hapo, Justine Masejo alimtaja mfanyabiashara mwingine anayeshikiliwa kuwa ni William Taitas maarufu kwa jina la Baraka Mkazi wa Ngulelo ambao walikamatwa jana majira ya saa 12 jioni katika eneo la tukio, Ngulelo.

Kamanda Masejo alisema kuwa wafanyabiashara hao wana mgogoro wa kugombea eneo ambalo lilitolewa uamuzi na mahakama kuu, kwamba Mollel ambaye amewekeza kituo cha Mafuta si Mmiliki halali wa eneo hilo lenye ukubwa wa ekari sabalililopo Ngulelo jijini Arusha.

Alifafanua kuwa ugomvi huu wa kutishiana kwa silaha na kuleta taharuku kwa mamia ya watu wa eneo hilo kukimbia hovyo hovyo uliibuka mara baada ya Mollel kumkuta Taitas akiwaamurisha wafanyakazi wa Kituo Cha mafuta kukabidhi mali mbalimbali kwa maandishi na waondoke eneo hilo.

Mollel baada ya kupata taarifa hiyo aliibuka ghafla katika kituo hicho cha mafuta na kutishia kumpiga risasi Taitas ambapo naye alichomoa silaha yake ndipo Mollel alipofyatua risasi hewani na kuibua taharuki eneo hilo na watu kutawanyika.

Alisema baada ya tukio hilo kutokea polisi walifika na kuwatia nguvuni wote na watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa na polisi huku silaha zao zikichukuliwa na jeshi hilo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz