Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tabora: Kiongozi wa dini avamiwa usiku, akatwa mapanga

Kamanda Abwao Kamanda Abwao

Wed, 9 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Tabora limethibitisha kunusurika kifo kwa kiongozi mmoja wa dini anayefahamika kwa jina la Sheikh Rashid Lupala, mkazi wa Tabora mjini ambaye anadaiwa kuvamiwa na watu wasiojulikana majira ya saa tatu usiku, wakati akitokea shambani kwake.

Inaelezwa kuwa, akiwa njiani anaendesha pikipiki, alitegewa kamba na kudondoka kisha akashambuliwa kwa mapanga.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao amesema bado wanaendelea na uchunguzi huku Baraza kuu la Waislam Tanzania Bakwata Mkoa wa Tabora wakilaani tukio hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live