Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taarifa za vigogo Six Telecoms kuwasilishwa Mahakama Kuu

54840 Pic+telecom

Tue, 30 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Upande wa mashtaka katika kesi inayowakabili vigogo wa kampuni ya mawasiliano ya Six Telecoms Limited akiwamo wakili maarufu,  Dk Ringo Tenga wameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wako kwenye taratibu za kuwasilisha taarifa Mahakama Kuu.

Wakili wa Serikali, Batilda Mushi ameeleza hayo Jumanne Aprili 30 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, ambapo amesema upelelezi umeshakamilika na taratibu zinazofuata ni kuwasilisha taarifa Mahakama Kuu kitengo cha uhujumu uchumi.

"Kesi imekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi umeshakamilika taratibu zinazofuata ni kuwasilisha taarifa Mahakama Kuu kitengo cha uhujumu uchumi,” amesema.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 10 itakapotajwa tena na washtakiwa wamerudishwa rumande kutokana na shtaka linalomkabili kutokuwa na dhamana.

Mbali na Dk Tenga, washtakiwa wengine ni Hafidhi Shamte au Rashidi Shamte ambaye ni mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo, mfanyabiashara na mkurugenzi wa kampuni hiyo, Peter Noni, mkuu wa fedha wa kampuni hiyo, Noel Chacha na kampuni ya Six Telecoms.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka sita likiwamo la utakatishaji fedha.

Katika kesi ya msingi, Dk Ringo ambaye ni mkurugenzi na mwanasheria wa kampuni hiyo na wenzake wanadai kuwa kati ya Januari 1, 2014 na Januari 14, 2016 Dar es Salaam walitoza malipo ya mawasiliano ya simu za kimataifa chini ya kiwango cha Dola za Marekani 0.25 kwa dakika kwa lengo la kujipatia faida isivyo halali.

Pia katika kipindi hicho wanadaiwa kuhujumu miundombinu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kutoza gharama chini ya kiwango na kushindwa kulipa Dola za Marekani 3,282,741.12 kwa TCRA kama malipo ya mapato.

Washtakiwa hao , wanadaiwa katika kipindi hicho walishindwa kulipa ada za udhibiti za Dola za Marekani 466,010.07 kwa TCRA.

Katika shitaka la utakatishaji wa fedha, Hafidhi, Noni,Tenga na Chacha wanadaiwa kuwa, walitumia ama walisimamia Dola za Marekani 3,282,741.12 wakati wakijua fedha hizo ni zao la makosa ya udanganyifu linalotokana na mashitaka yaliyotangulia.

Pia washitakiwa hao wanadaiwa kuwa waliisababishia TCRA hasara ya Dola za Marekani 3,748,751.22 (sawa na Sh. 8bilioni



Chanzo: mwananchi.co.tz