Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TLS Arusha watoa neno kuhusu sheria ya utakatishaji fedha

94723 TLS 1+PIC TLS Arusha watoa neno kuhusu sheria ya utakatishaji fedha

Thu, 6 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kanda ya Arusha kimeishauri  Serikali ya Tanzania kupitiwa  upya sheria ya utakatishaji fedha kwa maelezo kuwa siku za hivi karibuni imeanza kutumika vibaya.

Hayo yameelezwa na mwenyekiti wa TLS wa kanda hiyo, Elibariki Maeda katika siku ya sheria ambayo kitaifa inafanyika Dar es Salaam.

Amesema kwa kuwa makosa hayo hayana dhamana ni muhimu sheria itazamwe kiwango kinachodaiwa kutakatishwa na nia ya sheria ilikuwa inalenga nini.

"Kuna daktari ameshtakiwa kwa utakatishaji kwa kumtoa mimba msichana na kupokea 250,000," amesema

Amebainisha kuwa ni muhimu sheria kutaja viwango vya utakatishaji na mazingira ya yake ili kuzuia watu kukaa muda mrefu gerezani kwa kuwa kosa hilo halina dhamana.

Awali mkuu wa mashtaka Mkoa wa Arusha,

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
Abdalah Changula ametaka  kuimarishwa misingi ya haki jinai.

Changula amesema ni muhimu kabla watuhumiwa kukamatwa upelelezi uwe umekamilika ili kesi zisichelewe kuisha.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz