Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TAKUKURU yakamata sita, kwa rushwa ya uchaguzi

49845 Pic+takukuru TAKUKURU yakamata sita, kwa rushwa ya uchaguzi

Wed, 17 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Ilala imesema wamewahoji watu sita baada ya kubainika kuhusika na tuhuma za kutoa rushwa ili kupitishwa katika nafasi za uongozi.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Ilala, Christopher Myava ambapo amewataka wanachama wa vyama mbalimbali kuzingatia sheria na kuepuka vitendo vya rushwa hasa katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge na Urais.

Katika hatua nyingine taasisi hiyo imewafikisha mahakamani watumishi wawili kutokea ofisi ya Mtathmini Mkuu wa Serikali kwa makosa mbalimbali ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka yaliyosababisha hasara ya fedha kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 46.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live