Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TAKUKURU yadaka vishoka wanaotapeli watu

Vishoka Pc Data Kamanda wa TAKUKURU Mara akizungumza na waandishi wa habari

Fri, 27 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na nchini (Takukuru) Mkoa wa Mara imedai kuwepo kwa watu wanaojifanya kuwa ni maofisa wa taasisi hiyo na kuwatisha wananchi hususani watumishi kwa kuwataka kuripoti katika ofisi za taasisi hiyo kwa ajili ya mahojiano.

Maofisa hao feki wamekuwa na tabia ya kuwalazimisha watumishi hao kuwapa fedha kwa madai ya kuwasiadia kumaliza tuhuma zao ambazo wanadai zimefikishwa Takukuru kwaajili ya uchunguzi na hatua zingine za kisheria.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa taasisi yake katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita kwa waandishi wa habari mjini Musoma, mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mara, Hassan Mossi amesema kuwa tayari hatua za kuwasaka watu hao zimeanza.

Amesema kuwa mbali na kuwatisha kuripoti ofisi za Takukuru, pia matapeli hao wamekuwa wakiwatisha watumishi hao kuwa endapo hawatawapa fedha basi Takukuru itafanya uchunguzi katika ofisi zao kuibua maovu wanayodai kuwa na taarifa nayo.

Kutokana na hali hiyo amewataka matapeli hao kuacha mara moja tabia hiyo kwa maelezo kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo ambapo amesema kuwa ofisi yake tayari imepokea malalamiko zaidi ya nane kuhusiana na utapeli huo.

"Kuna watu tayari wametapeliwa na kuchukuliwa fedha. Wanampigia mtu simu na kumuomba afike nyumba Fulani. Hivyo watu wawe makini, sisi tuna namba yetu 113 ambayo mtu akipiga muda wowote tunamuhudumia na sio hii ya kukutana nje ya ofsi zetu," amesema.  

Advertisement Katika hatua nyingine, Mossi amesema kuwa katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita ofisi yake imefungua kesi sita mahakamani na hivyo kufanya jumla ya kesi zinazoendela mahakamani zilizopo chini ya taasisi yake hadi sasa kuwa ni 20.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live